Waziri Mchengerwa atoa siku tatu kwa Bodi ya Filamu Tanzania kutekeleza maelekezo yake
Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa leo Aprili 23, 2022 amefanya ziara ya kikazi kwenye taasisi ya Bodi ya Filamu nchini (TFB) na kujadili mikakati mbalimbali ya kuboresha na kuleta mapinduzi kwenye tasnia Filamu nchini ambapo ametoa siku tatu za kufanyia kazi maelekezo kadhaa aliyoyatoa. Mhe. Mchengerwa amesema tasnia ya filamu inazalisha ajira na kutoa mchango mkubwa kwenye taifa hivyoTFB inatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na kasi ili kuleta mapinduzi yanayositahili kwenye sekta hiyo hapa nchini. Akiwakilisha baadhi ya mikakati ya TFB, kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo, Mtendaji Mkuu wa Taasisis hiyo, Dkt. Kilonzo Kiagho amesema taasisi hiyo imejiwekea mikakati kabambe ambayo inaendana na miongozo mbalimbali ya Serikali ikiwa ni pamoja na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi. Ameitaja baadhi ya mikakati itakayoleta mageuzi makubwa kwenye tasnia hiyo kuwa ni pamoja na kuanzisha tozo la filam...
Comments
Post a Comment