FIFA KUENDELEA KUISAIDIA TANZANIA, YARIDHISHWA NA UTENDAJI WA RAIS SAMIA
Na John Mapepele Rais wa Shirikisho la Soka Duniani(FIFA) Gianni Infantino amesema FIFA itaendelea kuisaidia Tanzania kutokana na kuridhishwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Michezo. Akizungumza usiku wa kuamkia leo Agosti 10, 2022 mara baada ya kupokelewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Mohamed Mchengerwa katika kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro amesisitiza kuwa FIFA itaendelea kuisaidia Tanzania. Akiongozana na wachezaji mahiri wazamani waliopata kucheza katika makombe ya dunia na mwamuzi Corina amesema amefurahishwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tanzania. "Tayari FIFA imekwishatoa msaada wa ujenzi wa viwanja changamani Dar na Tanga lakini wako tayari kwa ajili ya kuongeza vituo katika kanda nyingine" amefafanua Mhe. Mchengerwa Aidha, Mhe. Mchengerwa amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa kwenye ambayo imesaidia Tanzania kupiga hatua duniani katika michezo. Mh...