Rais Samia awamwagia madola wachezaji Jumuiya ya Madola- Mhe Mchengerwa
Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Serikali inakwenda kutoa zawadi kwa wachezaji wote watakaoleta medali za mashindano ya madola yanayoanza nchini Uingereza hivi karibuni kama hamasa maalum kwa wachezaji. Amesema kwa mara ya kwanza kabisa Serikali imeandaa zawadi dola 10000 kwa mshindi atakayerejea na medali ya dhahabu na dola 7000 kwa mshindi wa medali ya fedha na mshindi atakayeshinda medali ya shaba atapata dola za kimarekani 5000. Mhe, Mchengerwa ameyasema hayo leo Julai 20, 2022 kwenye hafla ya kuwaaga wachezaji wa Tanzania wanaokwenda kushiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Uingereza. Katika hafla hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam amewataka wachezaji kuweka uzalendo mbele na kuwataka kurudi na medali. Amefafanua kuwa watambue kwamba dhamira ya Serikali kwa sasa ni kufanya mapinduzi makubwa ambapo amesisitiza kuwa watanzania wamechoka w...