Posts

Showing posts from June, 2022

Rami Tanzania mwenyeji Tuzo za (MAMA) MTV Africa Music Award 2023

Image
  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amekutana na kufanya mazungumzo na makamu wa Rais na meneja mkuu wa Paramount Africa and Peer Lead BET International, Monde Twala,  na kukubaliana kushirikiana katika kuiwezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa tuzo za MAMA- MTV Africa Music Award kwa mwaka 2023. Waziri Mchengerwa amekutana na Monde Twala Jijini Los Angeles   katika jimbo la California nchini Marekani wakati wa hafla ya utoaji tuzo za BET kwa mwaka 2022. Katika mazungumzo hayo Waziri Mchengerwa amemwelezea nia na sababu ya Tanzania kutaka kuwa mwenyeji wa tamasha hilo la utoaji wa tuzo hizo kubwa za burudani kwa Afrika, kuwa ni kuongeza ushawishi kwa vijana wa kitanzania kuendelea kufanya vizuri katika sekta za burudani pamoja na kuitangaza zaidi Tanzania na uzuri wake katika ulimwengu. Katika mazungumzo hayo pande zote mbili zimekubaliana  kuungana kwenye kutafuta washirika katika kuendesha tuzo hizo, na kuridhia kuwa maandalizi yaanze ma...

Tamasha kubwa la Utamaduni la mikoa yote kufanyika Dar

Image
  Na John Mapepele Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo imeanza kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan la kufanya Tamasha kubwa la kitaifa la Utamaduni ambalo linakwenda  kushirikisha zaidi ya wadau elfu ishirini. Akizungumza kwenye kikao cha maandalizi cha pamoja baina ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Saidi Yakubu amesema tamasha hilo la kihistoria linajumuisha mikoa yote ya Tanzania linatarajia kuanza Julai Mosi mwaka huu  katika uwanja wa Uhuru ambapo  maonesho mbalimbali ya  vyakula na ngoma za asili. Amefafanua kwamba Julai, 2, 2022  kutakuwa na matembezi  maalum ya kuzunguka jiji la Dar es Salaam kwenye madaraja yote  ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Kasssim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.  Kwa upande mwingine, Yakubu amesema siku ya  Julai 3, 2022...

Ubingwa wa Yanga umeleta mshikamano- Mhe Mchengerwa

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameipongeza timu ya Yanga kwa kutwaa kombe la katika ligi Kuu ya NBC katika msimu huu. Mhe. Mchengerwa  ameipongeza Klabu ya Yanga kwa kuchukua Ubingwa huo huku akipongeza mshikamano na furaha za mashabiki, ambazo wamezionyesha  wakati wa kukabidhiwa kombe hilo na mapokezi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. " Kwa aina ya shangwe za ubingwa zilizofanyika jana na leo ni sawa na zile za mataifa yaliyoendelea ya Ulaya. Hakika mpira wa miguu ni mchezo mkubwa na pendwa duniani ambao huwaunganisha watu pamoja na kuleta amani, mshikamano, furaha na umoja baina ya wananchi" Ameongeza kuwa watanzania zaidi ya 90% ni wapenzi wa mchezo wa soka na amesisitiza kuwa serikali itaendelea kufanya kila linalowezekana kuhakikisha inaboresha miundombinu ya michezo na kuleta usawa katika michezo hasa mpira wa miguu ili  kila mtanzania aweze kupata furaha.  "Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe...

Mhe. Mchengerwa awapongeza wadau kupaisha uchumi

Image
  Na John Mapepele   Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewapongeza wadau wa sekta za Sanaa na Burudani kwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye uchumi wa taifa.   Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2021 imeeleza iliyosomwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwigulu Nchemba imeeleza kuwa katika mwaka 2021 eneo la Sanaa na Burudani limechangia kwa asilimia 19.4 “Shughuli za kiuchumi zilikuwa na ukuaji mkubwa katika kipindi cha mwaka 2021 ni pamoja na Sanaa na Burudani (asilimia 19.4)” imefafanua sehemu ya taarifa hiyo. Katika kipindi cha mwaka 2020 eneo hilo lilichangia asilimia 13.7 hivyo kufanya ongezeko la asilimia 5.7 katika kipindi cha mwaka mmoja tu.  Wadau mbalimbali wa sekta ya sanaa na burudani wameipongeza Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa mikakati inayobuniwa na Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo ya kuinua na kuboresha sekta hizo katika kipindi kifupi. “Nimefarijika sana kusikia ...

TANZANIA NA MAREKANI ZAJADILI USHIRIKIANO SEKTA ZA SANAA NA MICHEZO

Image
  Na John Mapepele, Dar es Salaam  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa wakiambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi wamekutana na Balozi wa Marekani hapa nchini leo Juni 8, 2022 wamekutana jijini Dar es salaam na kujadili masuala mbali mbali ya sekta za ikiwa ni pa moja na ujio wa msanii mashuhuri wa uchoraji ,Ashley Collins hapa nchini. Wakizungumza katika  kikao hicho ambacho Mhe. Balozi  wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald Wright ameambatana na Afisa Uhusiano wa Ubalozi huo, James Rodriguez wamejadili pia ujio wa Timu ya wachezaji nguli wanawake ya mchezo wa kikapu wa ligi  ya NBA nchini Marekani  hapa nchini ambao watakuja Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wachezaji wanawake wa mchezo huo hapa nchini.  Waziri Mchengerwa amesema viongozi hao wamekubaliana  kuendeleza  malengo ya Royal Tour kwa kushirikiana zaidi  kwenye kuendeleza sekta  za sanaa na michezo ikiwemo kuendeleza...

TIMU ZA SERENGETI GIRLS NA TEMBO WARRIORS WAPEWA HESHIMA YA MASHUJAA TAIFA NA BUNGE

Image
  Na John Mapepele   Timu ya wanawake ya soka chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Girls) imeweka  historia  ya kuwa  timu ya  kwanza kupewa heshima na Bunge la Jamhuri ya Muungano kuingia  na kukaa kwenye viti vya mawaziri ndani ya bunge  baada ya kufuzu kuingia  mashindano ya dunia ikiwa ni heshima ya mashujaa wa Taifa kwa kazi kubwa iliyoifanya ambapo kesho ni zamu ya Timu ya soka ya Taifa ya Walemavu ya (Tembo Warriors) ambayo pia imefuzu  mashindano ya dunia ya soka kwa walemavu. Akiongea   mara baada ya kuketi eneo hilo rasmi la mawaziri, Waziri mwenye dhamana ya Michezo nchini. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema ushindi huo unatokana  na jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuiwezesha  timu hiyo katika kipindi chote cha  maandalizi wa  mashindano hayo. “Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kwa kutuwezesha, kututia moyo na kutufuatilia kwa karibu sana katik...

Serengeti Girls imeibeba Afrika- Mhe. Mchengerwa

Image
  Na John Mapepele. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema kwa mara ya kwanza historia imeandikwa kwa timu ya soka ya wanawake ya umri chini ya miaka 17 (Serengeti Girls) kuitoa kimasomaso Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla baada ya kufuzu kuingia akwenye mashindano ya dunia baada ya kuibamiza Cameroon jana kwenye mchezo wa marudiano uliofanyika Zanzibar. Akizungumza wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2022/23 ya Wizara yake bungeni leo, Mhe. Mchengerwa ametoa rai kwa timu zote za Taifa katika michezo mbali mbali, kuiga mfano wa Serengeti Girls kwa kupambana kufa na kupona, kwa ari na uzalendo kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa lao. Ameongeza kuwa Serengeti Girls  imetimiza  ndoto  ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na watanzania ya kuiingiza Tanzania kwenye  historia  ya kushiriki  kwenye  mashindano ya kombe la dunia ambapo haijawahi kutokea  katika  nch...

Mhe. Mchengerwa Ataja Makubwa ya Rais Samia katika Michezo, azindua mbio za CRDB Marathoni, Ajisajili kilomita 42

Image
  Na John Mapepele. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imekua mstari wa mbele siyo tu katika  kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika michezo  bali inashiriki moja kwa moja kuwekeza katika michezo kwa  kuwa inaamini kuwa michezo ni uchumi na biashara ambayo inatoa ajira nyingi kwa vijana. Mhe. Mchengerwa amesema hayo leo Mei 5, 2022 kwenye uzinduzi wa msimu wa tatu wa mbio za kimataifa za CRDB kwenye viunga vya Nyerere jijini Dodoma ambapo amewataka wakuu wote wa mikoa na wilaya nchi nzima kuhamasisha michezo kwenye maeneo yao ili kusaidia wananchi kujenga afya, kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza na kuinua uchumi wao na taifa kwa ujumla.  Aidha, amewaelekeza maafisa michezo na utamaduni katika kila mkoa na wilaya kuratibu mazoezi na mashindano ya michezo na sanaa ili kubaini na kuwatambua watanzania wenye vipaji kupitia program iliyoanzishwa na Serikali i...

Michezo na Sanaa kuwanufaisha wananchi- Mhe, Mchengerwa

Image
  Na John Mapepele  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Wizara yake ina mikakati kabambe ya kuendeleza sekta za michezo, utamaduni na sanaa ili  kuleta mapinduzi makubwa  yatakayowanufaisha wananchi katika kipindi kifupi ikiwa ni pamoja na kuboresha  tuzo za muziki na filamu   kwa wasanii. Akizunguza usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la The Dream Concert la Msanii nguli wa Hip Hop nchini Joseph Mbilinyi au jina maarufu la Mr. Two Proud au Sugu ya kutimiza miaka 30 kwenye tasnia na kuzindua kitabu chake kiitwacho “Muziki na Maisha” ambapo amesema Wizara yake inatarajia kufanya mambo makubwa ambayo mbali na kuitangaza Tanzania katika anga za kimataifa yatasaidia kuinua kipato cha wasanii na wanamichezo na kuinua uchumi wa nchi yetu. Amesema Wizara  pia ina mipango mingi na imekusudia kufanya mambo mengi makubwa  kwa maslahi ya tasnia ya sanaa nchini ikiwemo kuandaa mkutano mkubwa wa wadau wa muziki wa Afrika...